Menu Close

Wafanya-Miujiza / Workers of Miracles

      

Kas. Stewart

Ni nani wafanya kazi wa miujiza baada ya kufanyika mwili wa Kristo, dhabihu ya upatanisho juu ya msalabani na kupaa mbinguni? Jibu la Biblia na la Marekebisho ni, “Mitume na wengine wachache, na hivyo katika enzi ya mitume tu.” Hata hivyo, Wapentekoste na Wakarismatiki wangejibu, “Mitume na wengine wengi katika enzi za mitume, na wengi tangu wakati huo.” Wanamabadiliko wengi wanadai kwamba jambo hilo linajumuisha mitumena na manabii katika miaka zaidi ya 1,900 tangu kifo cha mitume 12 na Paulo.

Hebu tuangalie kitabu muhimu cha Agano Jipya katika swala hili, Matendo, tukianza na taarifa mbili zilizoeleza kuwa mitume 12 walifanya miujiza. Kwanza, “Maajabu na ishara mengi yalifanywa na mitume” (2:43). Pili, “miujiza na maajabu mengi yalifanyika kwa mikono ya mitume kati ya watu” (5:12). Miujiza hii haikutendwa na waumini (wa kawaida). Hapa hatusomi kuhusu kanisa la mapema lililofanya miujiza bali mitume wanaotenda miujiza!

Matendo yanaweka kumbukumbu ya miujiza kadhaa iliyofanywa na Mtume Petro: kuponywa kwa mtu aliyezaliwa kilema (3:1-4, 22), Kuuawa kwa Anania na Safira (5:1-11), kuponya au kufukuzwa kwa umati wa watu wengi ndani na karibu na Yerusalemu (15-16), kuinua Enea aliyepooza (9:32-35) na kufufuliwa kwa Tabitha aliye kufa. (36-42).

Kuna maajabu mengi yaliyofanywa na mtue Paulo yanatajwa katika Matendo. Alipofusha Elima mchawi wa Kipro (13:9-12). Katika Ikoniamu, Alifanya”ishara na maajabu” (14:3) na Barnaba, mmoja wa “manabii na walimu” katika kanisa la Antiokia ambaye alitumwa na Roho Mtakatifu (13:1-2); alimponya mwanaume mlemavu huko Listra (14:8-10); alimfukuza mbali mtabiri-mwanamke huko Filipi (16:16-18).Huko Efeso, Mungu alifanya uponyaji na kutoa mapepo kwa njia isiyo ya Kawaida ya “Vitambaa” za Paulo (19:11-12). Paulo alimfufua Eutiko kutoka kwa wafu katika Troa (20:9-12) na hakuwa na madhara yoyote kutokana na kuumwa na sumu ya nyoka katika Malita (28:3-6). Katika kisiwa hicho, alimponya Publio ugonjwa wa kuhara damu na homa,na wengine wenye walikua na magonjwa mbalimbali (7-10). Je, kuna watu wengine ambao walifanya miujiza isipokuwa wale ambao tayari wametajwa? Ndiyo, wanaume watatu. Kwanza, kulikuwa na Stefano, ambaye “alifanya maajabu na miujiza kubwa kati ya watu” (6:8). Alikuwa mmoja wapo wa mashemasi saba wa kwanza ambao mitume 12 waliwaweka mikono yao juu yao (1-6). Zaidi ya hayo, Matendo 7 inamuonyesha Stefano si tu kama shahidi wa kwanza wa Kikristo lakini pia nabii kwa ajili ya kupokea maono ya mbinguni ya Kristo aliyekwezwa (55-60).

Pili, Filipo alifanya miujiza katika Samaria (8:6-7, 13). Sio tu kwamba, alikuwa kama Stefano, aliyetawazwa kuwa shemasi na mitume (6:1-6) lakini pia, alikuwa kama Timotheo (II Tim. 4:5), Mwinjilisti (Matendo 21:8), akitumia kikao cha muda kisicho cha kawaida, ambamo mtu alitenda kazi chini ya kuwasaidia mitume wa karne ya kwanza (Efe. 4:11).

Tatu, baada ya Kristo kumtokea Paulo kwenye barabara ya Dameski, Anania alimponya katika upofu wake (Matendo 9:12, 17-18). Masihi ambaye hapo awali alimpofusha Paulo kimuujiza baadaye alimtuma Anania amrudishe uwezo wake wa kuona kimuujiza. Mungu hakutumia yeyotekati ya mitume 12 (wa awali) kwa jukumu hili,vinginevyo wapinzani wa baadaye wa Paulo wangedai kwamba alikuwa mtume wa mitumba (rej. Gal. 1-2). Badala yake, Bwana alizungumza na Anania katika maono (Matendo 9:10-16), na hivyo Pia akutuonyesha kwamba alikuwa nabii.

Basi ni nani Mungu alimtumia kufanya miujiza baada ya kuinuliwa kwa Mwana wake? Kitabu cha Matendo kinasema nini? Hawakuwa washirika wa kawaida kanisani. Bwana aliwatia nguvu mitume 12, hasa Petro, na mtume Paulo. Watu wengine wanne wametajwa: manabii Stefano, Anania na Barnaba na mwinjilisti Filipo. Wanaume hawa walikuwa na uhusiano mzurisana na mitume, kama wale waliowekwa rasmi na mitume 12 (Stefano na Filipo) au kufanya muujiza juu ya mtume Paulo (Anania) au kuandamana na Mtume Paulo katika safari yake ya kwanza ya umishonari (Barnaba). Kwa vifo vya mitume, na kwa wale waliowekwa pamoja nao au kufanya kazi pamoja nao au kufanya muujiza juu yao, siku za watenda miujiza wa miungu zimeisha.

Hili lafafanua kauli ya Paulo hamasishwa katika II Wakorintho 12:12: “Hakika ishara za mtume zilifanyika katikati yenu kwa uvumilivu wote, kwa ishara, na maajabu, na matendo yenye nguvu.” Baada ya yote, ikiwa katika siku zetu wote au baadhi ya Wakristo wote au baadhi ya wachungaji au wazee, wanaweza kufanya miujiza, jinsi gani, “maajabu” hayo ni “ishara za mtume”?

Miujiza katika enzi ya mitume ilikusudiwa kuthibitisha (1) Mitume wa Kristo na/au (2) injili ambayo walitangaza. Kwanza, Agano Jipya linasema juu ya miujiza kama ya kuhalalisha wajumbe wa mitume wa Kristo,”hao waliomsikia” (Waebra 2:3): “Mungu pia akiwashuhudia, kwa ishara na maajabu,na kwa miujiza mingi, na zawadi za Roho Mtakatifu sawa sawa na mapenzi yake” (4). “Maajabu” pia yalikuwa na kazi hii kwa habari ya Bwana mwenyewe,kama Petro alivyotangaza siku ya Pentekoste, “Enyi watu wa Israeli, sikilizeni maneno haya; Yesu wa Nazareti, mtu aliyekubaliwa na Mungu kati yenu kwa miujiza na maajabu na ishara, ambazo Mungu alitenda kwa yeye katikati yenu, kama ninyi wenyewe mjuavyo” (Matendo 2:22; taz.Yoh 3:2; 5:36; 9:16, 30-33; 10:25, 37-38).

Pili, miujiza ilithibitisha ujumbe wa mitume 12: “wakatoka, wakahubiri kila mahali, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo” (Marko 16:20). Hii ndiyo hali ya Injili iliyohubiriwa na mtume Paulo na nabii Barnaba aliyeandamana naye: “Kwa hiyo wakakaa (huko Ikonio) siku nyingi wakinena kwa ujasiri katika Bwana, ilishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao” (Matendo 14:3).

Hebu tushike sana mitume wa Agano Jipya na injili ya kitume ambayo waliyoitangaza: wokovu umo katika Kristo pekee kwa utukufu wa Mungu pekee (I Wakor.15:1-4)!

Show Buttons
Hide Buttons