Menu Close

Uhuru wa Hiari: Je, wokovu unategemea chaguo la mtu? / Free Will: Does Salvation Depend on a Person’s Choice?

    

Rev. Ron Hanko

Wakati wa Matenegenezo ya Kiprotestanti, Martin Luther aliandika kitabu chenye kichwa, Utumwa wa Wasia. Kitabu hiki kiliandikwa dhidi ya mtu mmoja aliyeitwa Erasmus na mafundisho yake kwamba mwanadamu ana hiari, yaani, uwezo wa kuchagua ikiwa kama ataokolewa au la. Luther alimwambia Erasmus kwamba swali hii kuhusu hiari lilikua suala muhimu Zaidi la Matenegenezo ya Kanisa. Alisema, “Wewe [yaani Erasmus] hujanitia wasiwasi na masuala ya nje kuhusu upapa, toharani, msamaha na kama vile, – mamabo madogo badala ya masuala… wewe na wewe peke yako,mmeona bawaba ambayo wote wana geukia, na wamelenga mahali muhimu…”

Licha ya yale Luther aliandika, fundisho la Erasmus kuhusu uhuru wa kuchagua limekuwa fundisho la Wanaprotestanti wengi siku hizi. Uhuru wa hiari ni:

  1. Kukataa utabiri. Kuamuliwa kunamaanisha kwamba mapenzzi ya Mungu (chaguo la Mungu) huamua mambo yote, ikijumuisha ni nani atakayeokolewa (Waefeso 1:3-6). Uhuru wa hiari hufundisha kwamba chaguo la mwanadamu ndilo jambo la kuamua katika wokovu.

  2. Kukana ukweli wa kibiblia kwamba Imani iokoayo ni zawadi ya Mungu (Waefeso 2:8-10). Uhuru wa hari hufundisha kwamba Imani ni uamuzi wa mtu mwenyewe kumwamini Kristo.

  3. Kukana ukweli kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya watu wake tu (Mathayo 1:21). Uhuru wa hiari hufundisha kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya wote bila ubaguzi na kwamba wokovu wao sasa unategemea Kumkubali kwao, yaani, juu ya chaguo la “hiari”.

Imani katika hiari pia inajionyesha yenyewe katika aina ya mahubiri na uinjilisti amabao unawasihi wenye dhambi kumpokea Kristo, amabao hutumia miito ya madhabahuni, rufaa, nyakati za maamuzi, kuinua mikono, na mbinu zingine kama hizo ili kuwashawishi kufanya hivyo. Mambo haya yote yanakisia kwamba wokovu wa mtu unategemea uchaguzi wake mwenyewe.

Tunaamini kwamba mapenzi ya mwanadamu yamo katika utumwa wa dhambi na kwamba si tu kwamba hawezi kufanya mema, lakini hawezi hata kutaka (kutaka) kufanya (Warumi 8:7-8). Hasa hawezi kufanya jambo jema Zaidi kuliko yote, la kuchagua Mungu na Kristo.

Kwa hiyo, tunaamini kwamba mwanadamu hawezi kumwamini Kristo isipokuwa “amewezeshwa kutoka mbinguni”.

Pia tunaamini kwamba hakuna mapenzi ya mtu, lakini mapenzi ya Mungu kuu na ya milele (Kuchaguliwa tangu awali) ni jambo lakuamua katika wokovu (Matendo 13:48; Wafilipi 2:13).

Ni nini basi, maana ya kuhubiri injili kwa wote? Ni “uweze wa Mungu uletao wokovu” (Warumi 1:16), njia amabayo Mungu huwapa Imani na toba wale wote ambao amewachagua tangu milele na kukombolewa Katika Kristo. Na iwe hiyo nguvu ya wokovu kwa wengi!

Show Buttons
Hide Buttons