Menu Close

Je, Kanisa Ni Mama Yetu? / Is the Church Our Mother?

       

Kas. Ron Hanko

Swali letu kwa suala hili linatoka kwa rafiki katika Amerika Kusini: “Mbali na kanisa kuwa bibi-arusi au mke wa Kristo, kulingana na Wagalatia 4:26 na mistari mingine … je, kanisa pia ni mama wa waumini au Wakristo?”

Maandiko kwa maneno mengi hayaliiti kanisa mama wa waumini. Hata hivyo, msemo ni, tunaamini, unathibitishwa na Maandiko. Ufunuo 21:9 yadokeza kwa ajili ya Yesu, kama kanisa ni bibi harusi wa Kristo, basi, kinachofuata ni kwamba yeye pia ni mama yetu.

Isaya 66:10-11 anatuhimiza, “Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni pamoja naye, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake; mpate kunyonya na kushiba kwa maziwa ya faraja zake; mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.” Yerusalemu lilikuwa ni jina la kanisa katika Agano la Kale na linaendelea kuwa jina la kanisa katika Agano Jipya (Waebra 12:22-24; Uf. 21:2). Isaya kwa hakika anaelezea Yerusalemu kuwa mama ya waamini, kwa hiyo.

Mstari uliotajwa na rafiki yetu wa Amerika Kusini, Wagalatia 4:26, ni karibu zaidi ya yote kwa rejea halisi kwa kanisa kama mama yetu: “Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, ambayo ni mama yetu sote.” Hapa tena, katika mfano, jina Yerusalemu ni jina la kanisa na kanisa linaitwa “mama yetu sisi sote.”

Kanisa ni mama katika maana ya kwamba yeye anatuzaa. Sio kanisa ambalo Hufanya kuzaliwa upya, kutuhesabia haki na kututakasa, lakini ni kupitia njia ya huduma yake kwamba Mungu hufanya kazi yake ya neema ndani yetu. Hivyo Paulo anawaita washiriki wa Kanisa, “Watoto wangu wadogo, ambao ninaonea utungu kwa ajili yao tena, mpaka Kristo aumbike ndani yenu” (Gal. 4:19).

Kanisa la Kikristo sikuzote limetambua usahihi wa jina hili. Padri wa kanisa Cyprian alisema,”Hakuna anayeweza kuwa na Mungu kama Baba ambaye hana kanisa kama Mama” (Umoja wa Kanisa, sura 6) na Calvin aliandika mara kadhaa katika taasisi zake za kanisa kama mama wa waumini. Hapa ni baadhi ya nukuu zake maarufu:

Nami nitaanza, basi, pamoja na kanisa, ambalo Mungu anapendezwa kuwakusanya wanawe kifuani mwake, si tu kwamba walishwe kwa msaada wake na huduma yake wakati wangali watoto wachanga na watoto, bali pia kwamba waweze kuongozwa na utunzaji wa mama yake mpaka watakapokomaa na hatimaye kufikia lengo la imani. ‘Kwa maana kile ambacho Mungu ameunganisha, si halali kutenganisha’ [Marko 10:9 p.], ili, kwa wale ambao yeye ni Baba ,kanisa liwe Mama kwao pia. Na hii haikuwa tu chini ya sheria bali pia baada ya kuja kwa Kristo, kama Paulo anavyoshuhudia wakati anapofundisha kwamba sisi ni watoto wa Yerusalemu mpya na ya mbinguni [Gal. 4:26] (4.1.1).

Lakini kwa sababu sasa ni nia yetu kujadili kanisa linaloonekana, hebu tujifunze hata kutoka kwa kichwa rahisi ‘mama’ jinsi inavyofaa, kwa hakika jinsi ilivyo lazima, kwamba tunapaswa kumjua. Kwa maana hakuna njia nyingine ya kuingia katika uzima isipokuwa mama huyu achukue mimba yetu katika tumbo lake, na kutuzaa, na kutulisha katika matiti yake, na Mwisho, isipokuwa tu kutuweka sisi chini ya ya uangalizi wake na uongozi wake yeye kuweka sisi chini ya uangalizi wake na uongozi mpaka, kuweka mbali mwili wa kufa, tukawa kama malaika [Matt. 22:30]. Udhaifu wetu hauturuhusu kufukuzwa kutoka shule yake hadi tumekuwa wanafunzi maisha yetu yote (4.1.4).

Jina hili “mama”limetumika vibaya, hasa na Ukatoliki wa Roma ambao hutumiajina hilo kisisitiza mamlaka yake kamili. Kwa sababu Kanisa ni mama yetu, kwa hiyo wanafikiri, nilazima tusujudie mamlaka yake kama tunavyoiinamia mamlaka ya Neno la Mungu: bila kujibakiza na bila swali. Hata hivyo, matumizi mabaya hayo ya jina hujibiwa kwa urahisi kwa kukumbusha kwa urahisi kwamba hakuna mama ambaye aliye mwema ambaye haji na Maandiko mkononi na ambaye hana mamlaka yake juu ya Neno hilo.

Ingawa tukikataa makosa ya Kiroma, kufikiria kanisa kama mama yetu hutumika kama ukumbusho wa baadhi ya mambo muhimu kuhusu kanisa. Ni ukumbusho wa umoja wa Kanisa la Kristo katika mataifa yote na historia yote. Waumini wana mama mmoja tu, ingawa Kanisa linaloonekana na kugawanyika. Sisi sote – haijalishi malezi yetu, rangi ya ngozi, utaifa, lugha, nk.- si tu kuwa na Baba mmoja lakini pia mama mmoja. Majina kama Yerusalemu na Sayuni ni majina ya kanisa, katika Agano la Kale na Agano Jipya (Wagal. 4:24-27; Waebra. 12:22-24), na ni mfano wa umoja huu waajabu, ambao unadumu kwa Muda mrefu zaidi nakupita wakati.

Jina mama linakumbusha kanisa na viongozi wake kwamba yeye lazima awe kama mama kwa washirika wake, na sio kama chunusi dhalimu na mwenye nyetea. Inatumika kama ukumbusho kwa washiriki kwamba Kanisa ni mahali ambapo wanapaswa kutarajia kulishwa, malisho vyema, kufarijiwa, kurekebishwa na kuongozwa (Isa. 66:10-11). Hawapaswi kuondoka upande wake, isipokuwa yeye katika udhihirisho wake unaoonekana inakuwa kahaba badala ya mama. Ingawa jina Mama halitumiki katika Ufunuo 22:17, wazo la kanisa kama mama yetu, ambaye kupitia kwake Mungu amemtoa kwa ajili ya watoto wake, kwa hakika linapatikana pale: “Na Roho na Bibi arusi wasema, Njoo. Kila mtu asikiaye hii naye aseme, Njoo. Na aliye na kiu na aje. Na yeyote Atakaye penda, na achukue maji ya uzima bure.”

Katika makanisa fulani, mkazo wote uko kwenye “kuokoa roho “lakini ni nini inachofanywa kwa wale ambao wameokolewa hivyo? “Mama” Kanisa hufanya kidogo au hakuna chochote kinachofanya kulisha na kutunza watoto wake.

Hakuna kinachosemwa kuhusu ushiriki wa kanisa katika uenezaji wa Injili, na wale ambao wanakuwa washiriki wa kanisa wameachwa bila kufundishwa na kuongozwa. Mkazo huo huo potofu kuhusu “kuokoa roho” mara nyingi husababisha kupuuzwa kwa wale ambao wamekuwa washiriki wa kanisa kwa muda mrefu, hasa wazee, wajane, wagonjwa na maskini. Inasababisha mara nyingi sana kuwapuuza vijana pia. Ingawa chini ya uangalizi wa kanisa mama, wanabaki bila kufundishwa na haishangazi kwamba wanaenda zao wenyewe mwishowe.

Kama mama yetu, kanisa inastahili heshima na upendo na utii wetu. Wakristo wanapaswa kujiweka chini ya uangalizi wake, “kudumisha umoja wa Kanisa; wakitii haowenyewe kwa mafundisho na kwa nidhamu yake; wakiinamasha shingo zao chini ya nira ya Yesu Kristo; tena tukiwa washirika wa mwili mmoja uleule, wakihudumu katika kuwajenga ndugu, sawasawa na talanta alizopewa na Mungu” (Kukiri wa Belgic 28).

Wakati mama yetu anapokuwa mgonjwa sana, kama anavyokuwa wakati mwingine, hatupaswi mumwacha mara moja, bali lazima tutafute uponyaji wake na ustawi wake, kupitia maombi tukisimama kwa ajili ya ukweli na, ikiwa ni lazima, matengenezo ya kanisa. Mara nyingi sana wale wote ambao hawangefikiria kumwacha mama yao wa asili hukata tamaa kwa mama kanisa wakati yeye ni mgonjwa na kupungukiwa kufikia kiwango cha afya ya kiroho kilichowekwa na Neno la Mungu. 

Show Buttons
Hide Buttons