Menu Close

Alitunzwa na Mwenyezi Mungu (na Malaika wake!) / Kept by God (and His Angels!)

    

Kas. Angus Stewart

Malaika watakatifu wanahusishwa husishwa na kuzaliwa kwa Bwana Yesu. Katika Luka 1, malaika Gabrieli anakuja hekaluni kumwambia Zakaria, kuhani mzee,kwamba yeye atakuwa baba wa Yohana Mbatizaji,mtangulizi wa Kristo; miezi sita baadaye, Gabrieli anamtangazia bikira Maria kwamba atazaa Mwana wa Mungu aliye mwilini. Mara tatu Yusufu anaongozwa na malaika katika ndoto kwenye Mathayo 1-2: aliambiwa amwoe Maria, amkimbie Herode (ambaye alishawishiwa na ibilisi; Ufu. 12:4) alikwenda Misri miezi michache baada ya Kristo kuzaliwa mjini Bethlehemu, na kurudi Israeli baada ya kifo cha Herode.

Zaidi ya hayo, siku ileile ambayo Kristo alizaliwa, malaika aliwatokea wachungaji fulani karibu na Bethlehemu ili kutangaza kuzaliwa kwa Mwokozi. Ndipo malaika mmoja akaungwa mkono na wengi wa wenzake: “Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu mapenzi mema kwa watu” (Luka 2:13-14). Hii ndiyo tu Biblia inataja malaika duniani wakimwabudu Aliye Juu Zaidi; kila mahali, sifa ya malaika inatajwa,inatukia mbinguni. Kwa kushangaza, Maandiko yanafunua kwamba malaika waliopelekwa Bethlehemu walikuwa wakimwabudu Mungu; hakuna hata mkaribishaji mmoja wa mbinguni aliyeshindwa kumsifu Mfalme huyo aliyezaliwa: “Hapo alipomleta yule mtoto wa kwanza ulimwenguni, asema,Na malaika wote wa Mungu wamsujudie” (Ebra. 1:6).

Karibu na mwanzo wa huduma yake, malaika walimhudumia Kristo baada ya majaribu yake katika jangwa (Math. 4:11); karibu na mwisho, malaika aliimarisha katika hali yake ya mwanadamu wakati wa maumivu yake katika bustani ya Gethsemane (Luka 22:43). Alikuwa ni malaika aliyeliondoa jiwe kutoka kwenye kaburi laKristo (Mt. 28:2) Lakini Yesu hakumwacha Petro nje (maana Bwana aliyefufuka alikuwa amekwisha ondoka),bali kwa ajili ya watu wake,ili wafuasi wake waone kwamba alikuwa ameondoka. Macho ya mwisho ya wanafunzi wa Yesu Kristo kupaa kwake mbinguni, mikono iliyonyooshwakwa baraka iliambatana na kuelezwa na malaika wawili (Matendo 1:10-11).

Mwana wa binadamu si tu mara nyingi alisema kuhusu malaika wazuri na walioanguka; Pia alipigana na Ibilisi na mapepo yake, hasa wakati wa majaribu yake, kwa kupuliziwa na kusulubiwa kwake.

Yohana 1:51 hasa inadhihirisha jambo hili, kwa kuwa Yesu alimwambia Nathanaeli na Filipo, “Baada ya hapo mtaona mbingu zimefunguliwa, na malaika wa Munguwakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.” Huduma wa malaikajuu ya Kristo, mbali na mifano michache iliyotolewa, haikuwa inayoonekana na hata hivyo hawakuonekana na wanafunzi kabla ya ufufuo wa Kristo, kwa sababu ama walikuwa hawapo au wamelala wakati malaika walipotokea. Lakini wao na sisi, kwa imani, tunaweza kuelewa kitu chahuduma ya kuendelea,ulinzi na uongozi wa Mungu wa mbinguni na nchiuliotolewa kwa ajili ya Mwana wake aliyefanyika mwili kupitia huduma yao asiyeonekana.

Marejeo ya Bwana wetu kwa malaika waliopanda na kushuka juu yake ilikuwa ni uvutio kwa ndoto ya Yakobo katika Betheli (Mwa. 28:12). Malaika wanaomlinda Kristo, kichwa chao, wakiwa hawaangalii kwa macho Yakobo au Israeli na “watoto” wote wa Kristo (Mt. 18:10; Ebra. 1:14). Kupitia kwa wajumbe wake wa mbinguni, Mwenyezi husaidia imani yetu dhaifu kwa kutuhakikishia kuwepo kwa agano lakemwenyewe pamoja nasi, akitulinda na maovu, kulingana na mapenzi yake ya milele na uhuru. Mungu wa Utatu-anayetukumbusha utunzaji wake na malaika wake – na awalinde ninyi, mwamini, kwa neema na Roho wa Yesu Kristo mwaka wa 2012. “Bwana atakulinda toka kwako, na kuingia kwako tangu wakati huu na hata milele” (Zab. 121:8).

Show Buttons
Hide Buttons