Menu Close

Asili ya Miujiza ya Mitume / The Nature of Apostolic Miracles

       

Kas. Stewart

Katika toleo la lililopita, tulijulisha ishara za mtume (II Wakor. 12:12) na kuorodhesha aina mbali mbali za miujiza (Mt. 10:8; Marko 16:17-18). Lakini Vipi kuhusu miujiza inayodaiwa na Wapentekoste na Wakarismatiki katika siku zetu wenyewe? Mengi yao hayawezi kuthibitishwa, kama vile “uponyaji” wa migongo mbaya na maumivu ya kichwa au magonjwa ya kisaikolojia. Je, mtu anathibitishaje kwamba mtu kwa kweli alikuwa na maumivu haya, kwamba hana tena maumivu hayo na kwamba ilitokana na muujiza uliofanywa Mkarismatiki? Namna gani kufanya miujiza yao “migumu” kama vile kufufua watu kutoka kwa wafu, kuwasafisha wenye ukoma, na kuwafanya watu waliozaliwa vilema kutembea, n.k.? Madai kuhusu mambo haya ya Wapentekoste na Wakarismatiki ni nadra, na ni wachache wanaosimama hata kwa uchunguzi mdogo.

Victor Budgen anasimulia hadithi hii ya kufurahisha ya mkutano wa uponyaji huko London: “katikati ya mkutano wa hadhara wa Albert Hall Mwenyekiti alitangaza kuwa mtu fulani katika kutaniko ambaye aliyekuwa mgonjwa alikuwa katika chumba cha ambulensi cha St. John, na kama kulikuwa na daktari ndani ya nyumba angeomba aende huko haraka” (Karismatiki na Neno la Mungu, uk. 100). Ni wapi imani ya mwenyekiti na waliohudhuria katika nguvu za uponyaji zaviongozi wa Karismatiki? Kwa nini walihitaji kurejea kwa madaktari?

Miujiza ya II Wakorintho 12:12 ilikuwa halisi na isiyoweza kukanushwa, kwa kuwa ilibidi iwe ili kutumikia hoja ya Paulo. Ni wazi, wakati alipokuwa Korintho kwa muda wa miezi 18 (Matendo 18:11), mtume alikuwa amefanya miujiza mingi ambayo iliwafanya wale waliwatazama kushangaa na kuwaelekeza kwenye ukweli wa Injili ambayo alihubiri: Yesu Kristo alisulubiwa na kufufuka kwa ajilli ya wenye dhambi! Kando na ushahidi wa miujiza iliyofanywa na Paulo katika kitabu cha Matendo Ya Mitume na IIWakorintho 12:12, Mtume alizungumzia miujiza yake ya Galatia katikati mwa Uturuki (Gal. 3:5) na hata kutoka Yerusalemu hadi kaskazini na magharibi hadi Iliriko, takribani Yugoslavia ya zamani (Warum. 15:19).

Wapinzani wapagani, Wayahudi wasioamini, na mitume wa uwongo, wangependa sana kuweza kukana maajabu ambayo Paul alifanya. Lakini, kama miujiza ya Kristo (Yohana 11:47), na ya Petro na Yohana (Matendo 4:14-16), matendo makuu ya Paulo hayakuweza kupingwa.

Ona, kwanza kwamba mitume waliwaponya watu kabisa. Ainea alipooza alikuwa amelazwa kitandani kwa miaka minane. Petro alitangazia, “Yesu Kristo anakuponya,” naye akainuka na kutandika kitanda chake (Matendo 9:32-35). Ainea hakuonyesha tu maendeleo au kuwa na maendeleo. Badala yake, alikuwa na nguvu isiyoharibika katika viungo vyake.

Pili, mitume waliponya watu mara moja, kama yule mtu kilema wa Matendo 3. Hakukuwa na haja ya matibabu yoyote baadaye au mchakato wa ukarabati.

Tatu, mitume walimponya kila mtu aliyekwenda kwao kutafuta uponyaji (kwa mfano, Matendo 5:12-16). Hawakujaribu kumponya mtu lakini wakashindwa, na kisha kumlaumu mgonjwa: “Wewe hukuwa na imani ya kutosha!” Hawa ni tofauti kabisa na wale wanaodhaniwa kuwa waponyaji wa siku zetu!

Baada ya zaidi ya karne ya Upentestosti (pamoja na Karismatiki na Ukirismatiki mamboleo), iko wapi miujiza yao isiyoweza kukanushwa? Wagonjwa wengi walidaiwa kuponywa lakini niwagonjwa kama walivyokuwa. Wengine wamefuata mikutano mingi ya uponyaji wakitafuta matibabu lakini hata hawajadai kwamba wamepata uponyaji. Kumekuwa na makundi ya wadanganyifu na wanahatari. Jina la Kristo limekuwa limekashifiwa mara kwa mara mbele ya ulimwengu na matapeli hawa na bado watu wanaodanganyika kwa urahisi bado wanalikubali.

Alikuwa tofauti kama nini na mtume Paulo! “Hakika ishara za Mtume zilidhihirishwa kwenu katika uvumilivu wote, kwa ishara, na maajabu, na matendo yenye nguvu” (II Wakor. 12:12). Paulo anawaambia Wakorintho, kwa kweli, “Mliona nguvu wa Mungu ndani yake, mkashangaa kuona miujiza iliyotendwakwa mikono yangu. Hizi ni ishara za ofisi yangu ya kitume ─kwamba ninyi wenyewe mmeshuhudia kwa macho wala hamuwezi kuzikana. “Kwa upande mwingine, miujiza ya kujifanya na maponyo yasiyokamilika (bora zaidi) ni ishara za mlaghai, mwalimu wa uwongo mwenye injili ya uwongo, mara nyingi yule anayetaka kuwadanganya watu.

Kasisi mmoja anaeleza jinsi mtu anayejua wakati ambapo “Ameguswa kwa Uponyaji.” “Kwa kawaida utahisi joto kali kwenye mwili wako wote. Kisha baada ya dakika chache, wengi watahisi amani ya ajabu isiyo ya kawaida kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. Utajua wakati hii inatokea, linahisiayapendeza sana. Ni kama mbingu duniani. Utajua hilo litatojkea na hutakuwa na shaka yoyote. Utajua ni Roho Mtakatifu wa Yesu Kristo anayekugusa … Wakati mwingine utahisi upepo kwanza. Kweli!!!! Kama tu upepo halisi au upepo mdogo unaozunguka, hata katika chumba kilichofungwa kabisa. Wakati mwingine utahisi kama ni blanketi joto ya nishati amefungwa kuzunguka mwili wako wote. Hilo linapotokea, ni kama mavazi yasiyo ya kawaida. Inahisi kama sehemu yako kikamili. Nyakati nyingine utaskia harufu ya jasmini ya mbinguni au manukato mengine mazuri ajabu. Utajua harufu hii ni ya mbinguni na takatifu wakati inapojidhihirisha katika ujazo wa Roho Mtakatifu. Iwapo utawahi kunusa manukato hiyo ya ajabu, unakua na ziara maalum ya ziada kutoka kwa Bwana Yesu. Bila ya shaka yoyote mtawatambua mtakapozinusa.”

Je, ni kitu gani kinachoweza kufanywa kutokana na upumbavu huu wote usio wa Kibiblia? Ni wapi jambo kama hiki katika Maandiko yote matakatifu? Je, umeona ni mara ngapi mwandishi anazungumzia jinsi “inavyohisi” (mara sita katika fungu lililo juu)—hisia za joto au amani au upepo au blanketi au nguo zinazofaa kabisa—au “harufu” (mara nne)—Jasmini ya mbinguni au manukato nyingine ya ajabu?(Wafumbo wa Roma Katoliki mara nyingi huzungumza kutembelewa kwa kimmungu katika lugha inayofanana.) Jambo la kushangaza ni kwamba, hata haisemi kuwa unajua umeponywa kikweli! Wapendwa, ishara ya kweli ya mtume wa kibiblia ni uponyaji halisi bila mumbo-jumbo yoyote katika aya iliyotangulia,kama II Wakorintho 12: 12 na Agano Jipya hufundisha! 

Show Buttons
Hide Buttons