Menu Close

Ukuu wa Mungu

Rev. Gise Van Baren

Watu wengi siku za leo hukana kwamba Mungu anatawala mambo yote. Wanaendelea kutembea katika ujinga wao kwa kukataa ushuhuda dhahiri wa Biblia. Wakristo wengi pia huonekana kutokuwa na hakikisho la uweza na utawala wa Mungu. Wako na utayari kukubali kuwa Mungu anaokowa wenye dhambi, lakini wanamashaka iwapo Mungu anauwezo wa kukamilisha kikamilifu malengo Yake. Wanakubali kuwa Mungu hupeana mambo yote mazuri, lakini wanasita kukubali kuwa Mungu huruhusu vita na magojwa. Wako nautayari wakusema kuwa Mungu huongoza watu wazuri, bali wanasita kukiri kuwa watu waovu pia wako chini ya utawala na uongozi Wake.

Moja wapo ya kweli ya kihistoria inayo ungamwa kikamilifu na makanisa ya Warifomu na Wakalvini ni kuwa Mungu wetu ni Mkuu. Tunaposema Mungu ni Mkuu tunamaana kwamba Yeye ni mtawala wa kila kitu na anatawala kwa ukamilifu wote, Yuko juu ya kila kitu na anaongoza kila kitu. Utawala na ukuu wa Mungu si punguani. Hajakabidhiwa utawala huu na mutu yeyote. Ukuu Wake hauna kipimo wala kikomo, Mungu ana haki ya kutawala. Mungu si mtawala wa kidemokrasia anayatawala kwa mapenzi ya watu. Utawala Wake na mamlaka Yake, hutokana na Yeye tu. Mungu hudhihirisha wazi utawala huu juu ya uumbaji Wake. Yeye pekee ni Mkuu. Hakuna kitu kinacho kwepa utawala Wake.

Huu ni ukweli dhabiti. Bila ukweli huu, au tunapoharibu ukweli huu, tutapeana fursa watu kuja na mafundisho na imani zilizo kinyume na Neno la Mungu. Angazia jambo hili katika mwangaza wa kile Biblia inafundisha.

Kwanza kabisa ukuu wa Mungu huunganisha ukweli kwamba ameumba ulimwengu wote kwa uweza wa Neno Lake. Mungu ndiye anayelinda na kushikilia ulimwengu na maumbile Yake yote. Ulimwengu ni mkubwa mno kiasi ya kwamba wanadamu hawezi kuelezea mwazo wake wala mwisho wake. Idadi ya nyota ni kubwa na haziwezi kuhesabika. Kuna wale wanaodai kuwa ni wajinga kuhusiana na chanzo cha ulimwengu. Wengi wanasema pengine ulimwengu ni wa umilele. Lakini Biblia inatueleza kwa urahisi, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwanzo 1:1) na Waebrania 11:3 inasema, “Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.” Hebu waza! Mungu aliumba ulimwengu mkumbwa, na Yeye yu juu ya ulimwengu, na hakuna vile umemfanya Yeye kupunguwa. Pia Sulemani aliomba akiweka wakfu hekalu mjini Yerusalemu, “Lakini Mungu je! Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga! (I Wafalme 8:27).

Mungu aliumba kila kitu kupitia uwezo wa Neno Lake. Lakini ukuu Wake si katika uumbaji tu. Yeye ni mkuu kwani anaongoza na kutawala kila kitu kinachotendeka. Mungu aliweka vipimo vya bahari: “Ayubu 38:8, “Au ni nani aliyefanya bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni?” Huzifunika mbingu kwa mawingu, Huitengenezea nchi mvua, na kuyameesha majani milimani (Zaburi 147:8). Mungu ndiye anyeongoza kila tone la mvua kunyesha atakapo na pia kila wingu kutanda kwa raha Zake na vile atakavyo. Uweza wa Mungu upo juu ya ndenge wa mbinguni na juu ya nywele zinazo anguka toka kichwani mwa mtu. Yesu akasema, “Je, mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yetu, lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote” (Mathayo 10:29-30).

Lakushangaza zaidi, ngawaje hupingwa na wengi, ni kuwa nguvu za Mun gu huungoza vita, shida, magonjwa na upepo unaokuja duniani. Mungu hatumi amani pekee, bali pia huruhusu vita. Mungu hupeana afya na pia hutuma magojwa na kifo. Mungu anasema katika Isaiah 45:7 “Mimi naiumba nuru, na kuihuluku giza, mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya, Mimi ni Bwana, niyatendaye hayo yote.” Pia tunasoma katika Zaburi 46:8, “Njoni myatazame matendo ya Bwana, jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.” Wakristo wanaposikia au kukumbana na dhoruba na mafuriko makubwa, na kuathiriwa na uharibifu wa magonjwa, wanapoona uangamivu wa vita, wapaswa kuwa na ukiri huu, “Mkono wa Bwana umetenda na kuongoza haya yote!”

Kuna ajabu nyingine tokana na ukuu wa Mungu. Utawala wake u juu ya watu waovu. Ndio, utawala wake u juu ya shetani mwenyewe. Imesemwa kwamba Mungu huongoza na kuwashawishi watu wazuri tu, bali watu waovu na shetani wapo nje ya utawala Wake. Watu husema kuwa Mungu anao uwezo wakutatiza mipango miovu na nguvu za giza, bali mamlaka hizi hazipo chini Yake. Iwapo mtazamo huu ni kweli basi kutakuwa na upungufu mkubwa wa ukuu wa Mungu. Ukweli ni kwamba Mungu ni mtawala wa waovu wote. Hawawezi kuinua kidole, na kutekeleza vitendo viovu hata kimoja, bila Mungu kuruhusu, kwani wako chini ya utawala wake.

Ukweli huu unaonekana dhahiri katika Maandiko. Tunasoma katika Kutoka 3-4, ya kuwa Musa, ambaye mwanzoni alitoroka toka Misri, alikuwa anachunga kondoo wa baba mkwe wake, Yathro. Hii imekuwa kazi yake kwa miaka 40. Mungu akamtokea na kubadilisha maisha ya Musa. Mungu alikutana naye katika kichaka kinacho waka moto na hakikuteketea nyikani, na kumuagiza kuenda kwa Farao na kumwambia kuwaachilia watu wa Mungu. Kisha Bwana akamwambia Musa, “hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanya mble za Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako, lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao”. Ni kweli kwamba mwanzoni moyo wa Farao ulikuwa mgumu, na kisha Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu. Kabla Farao hajatambua kuhusu uwepo wa Musa, Mungu alisistiza, “Nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu” (Kutoka 4:21). Matukuo ya kitendo hiki cha Mungu, Farao aliufanya moyo wake kuwa mgumu. Hata ingawa Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, farao mwenyewe anawajibika na anapata hukumu kuu, pitia mapigo kumi kwa ajili ya dhambi yake.

Kwa nini Mungu aliufanya Moyo wa Farao kuwa Mgumu? Mtume Paulo anapeana jawabu katika Warumi 9:17, “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.”

Matukio mengine yametajwa na Maandiko. Kuna habari ya 1 Wafalme 22 pale ambapo Ahabu alitafuta ashauri pitia manabii wa uongo kuhusiana na mipango ya kuwapiga vita Shamu. Manabii hawa wa uongo walimshawishi kwenda katika vita, na kumpa hakikisho la ushindi. Bali Ahabu alipo muita nabii wa Bwana Mikaya. Mikaya alimueleza Ahabu kwamba ni Mungu aliyeweka roho ya uongo midomoni mwa manabii wa uongo ili kuweza kumshawishi Ahabu na kumuongoza katika uangamivu vitani. Mungu alikuwa mkuu juu ya manabii wa uongo.

Bado kuna habari ya ziada, hata shetani yuko chini ya utawala wa Mungu. Ushahidi wa kutosha na uliowazi kuhusu habari hii unapatikana katika kitabu cha Ayabu. Katika mlango wa kwanza, tunasoma shetani akatokea mbele za Mungu. Mungu akamkumbusha shetani kwa habari ya Ayabu aliekuwa mtu mkamilifu na uelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Nyosha mkono wako sasa naye atakukufuru mbele za uso wako. Mungu akamwambia Shetani katika mstari wa 12, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako, lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Kwa hiyo Mungu alimpa Shetani uweza kwa kipimo kutekeleza mipango yake miovu ili kumfanya Ayubu kumkufuru Mungu.

Bado kuna suhahidi mwingi wakutufanya tushangae kuhusu ukuu wa Mungu unaofunuliwa na Maandiko. Mungu mkuu pitia nguvu zake pekee, huwaokoa watu wake kutoka kwa dhambi na mauti na kuwaleta katika ufalme Wake mbinguni. Wengi wa wahubiri hudai kuwa Yesu anasimama nje ya moyo wa mwenye dhambi na anaendelea kubisha mlangoni. Uwamuzi wakuokoka unapaswa kuchukuliwa na mtu mwenye dhambi. Mbali hili si fundisho la Maandiko. Katika Yeremia 31:18-19 tunasoma hivi, “Umeniadhibu, nami nikaadhibika, unigeuze, name nitageuzwa, kwa maana wewe u Bwana, Mungu wangu. Hakika baada ya kugeuzwa kwangu, nalitubu, na baada ya kufundishwa kwangu, nalijipiga mapajani, nalitahayarika, naam, nalifadhaika, kwa sababu naliichukua aibu ya ujana wangu.” Tunasoma kuhusiana na habari ya mahubiri ya umisheni ya Paulo na Barnaba, “Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini” (Matendo 13:48). Katika safari nyingine yaumisheni, Paulo alihubiri kwa wanawake walikuwa wanakutanika kuabudu kando ya mtu karibu na Filipi. Mmoja wa wanawake hao, Lydia, akaamini. Kuhusiana naye tunasoma hivi, “Ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yalionenwa na Paulo” (Matendo 16:14).

Zaidi, ni ukuu wa Mungu ulioonekana katika kusulubishwa kwa Yesu Kristo. Mtu anapotazama matukio pale msalabani, mtu anaweza kusukumwa kusema kwamba matukio hayo hayakuwa mkononi mwa Mungu. Inaweza kuonekana kana kwamba mambo ya matukio hayo hayakuwa katika utawala wa Mungu. Ni kana kwamba Shetani alikuwa karibu kupata ushindi. Lakini sivyo ilivyo fanyika. Mambo yote yalikuwa chini ya utawala wa Mungu pale msalabani. Kilichotokea, kiliambatana na makusudi makubwa ya Mungu. Petro aliwaeleza umma ya watu siku ya Pentekoste kwa kusema, “Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua” (Matendo Ya Mitume 2:23). Mungu alikusudia kifo cha msalaba ni lazima, bali ni watu waovu walimchukuwa wakamsulubisha Kristo. Mungu akatumia matendo maovu ya watu wabaya kutumiza makusudio yake makuu.

Ni katika ukuu Wake ambapo anawalinda watu wake katika wokovu anaowapa. Tunasoma katika Wafilipi 1:6, “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.”

Ukuu wa Mungu umefunua ya kuwa anatawala kikamilifu na utawala Wake uko juu ya kila kitu katika kuwaokoa watu Wake kutoka dhambini na kuwaleta katika ufalme Wake wa Utukufu.

Je, ni muhumu Wakristo waaminifu waendelee kusimama na kufundisha ukuu wa Mungu kama inavyofunuliwa na Maandiko. Ndio! Sababu kuu kwa nini ulimwengu upo ni kwa ajili ya Jina la Mungu kutukuzwa. Kila kilichotukia, kila kitakachotukia, kinapaswa kuhitimisha kusudio hilo la kumtukuza Mungu. Hakuna mtu au kitu kinapaswa kuiba ukuu wa Mungu.

Ni alama ya mafundihso mapotofu kuwa ukweli wa ukuu wa Mungu huyeyushwa. Mwanadamu atatanguliza kile kinacho mtukuza mwandamu, kinachotukuza uweza wa mwanadamu na nguvu zake, na kile kinacho mpongeza mwanadamu kuwa anauwezo wakufanya mambo na bila kuhitaji kitu kutoka kwa Mungu. Mwandamu atajaribu kujiondoa toka kwa utawala wa Mungu kwa kupendekeza kuwa wengine walio nje ya Mungu, walio na uwezo wakujitawala.

Ni alama ya Mkristo mwaminifu na kanisa la kweli kuamini na kukiri ukweli wa maandiko kuhusu ukuu na utawala wa Mungu. Mafundisho yote, kila ukiri, unapaswa kuwa chini ya ukweli wa ukuu wa Mungu. Kila kinacho zuia ukweli huu kwa njia yoyote kinapasw kupigwa na kukataliwa. Fundisho la kweli linapaswa kuambatana na kufunua ukweli kuwa Mungu ndiye Mkuu pekee.

Mkristo anapaswa kuishi na kutembea akitambua ukweli huu. Mara kwa mara ni rahisi yeye kuwaza kuwa anajitawala na hayupo chini ya uwezo na mamlaka ya Mungu. Hatafuti uso wa Mungu katika sala, kama impasavyo. Hasimami na ufalme wa Mungu kama mototo mwaminifu wa Mungu impasavyo. Hufurahia ulimwengu na tamaa yake yote. Mtu huyu huishi kana kwamba Mungu si Mkuu.

Ukweli kuhusu ukuu wa Mungu unashangaza! Mungu wangu ndiye anayesikia na kujibu sala zangu. Mungu wangu anaongoza mambo yote kwa ajili ya wema wangu (Warumi 8:28). Kwa kuwa Mungu wangu ni mkuu, hakuna janga ama ajali inayonipata. Mambo hayafanyiki kwa ajili wala kwa bahati nasibu. Nataka nikae nyumabani wa Bwana siku zote za maisha yangu. Mungu wangu mkuu ananiangalia pitia mwana wake Yesu kristo.

Ukweli huu ni faraja kubwa, na hakikisho kwa wakristo wanaojua na kukiri ukuu wa Mungu. Hakuna kitu kitakacho nitenganisha na upendo wa Mungu. Kwani Mungu anasema kwa Neno Lake, “Kwani nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, waka wenye mamlaka, wala yaliopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo. Wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 8:38-39). Hii ni kwa sababu Mungu ni Mungu mkuu. Asante Mungu kwa Ukuu wako!

Show Buttons
Hide Buttons