Menu Close

Umoja wa Kanisa / The Unity of the Church

         

Kas. Angus Stewart

Umoja wa kanisa umeelezwa katika Imani ya Mitume: “Naamini Kanisa takatifu, la Kikatoliki” (umoja), na kufundishwa, kwa mfano, katika Waefeso 4:4-6: “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu; Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja …”

Kanisa moja la Kristo ni kiumbe hai (“mwili mmoja”) na kichwa kimoja, Yesu Kristo (“Bwana mmoja”), na kanuni moja ya uhuishaji, Roho Mtakatifu (“Roho mmoja”), ambayo huabudu na kutumikia Mungu mmoja wa Utatu, Baba Mwana na Roho Mtakatifu (“Mungu mmoja”).

Mahali pa kina kabisa cha umoja wa kanisa ni kwamba Mungu mwenyewe ni mmoja (“Mungu mmoja”). Hivyo, Kanisa linaweza kuwa, moja na si mbili au zaidi. Umoja wa Kanisa uliamriwa milele na Mungu, maana “Yeye ametuchagua katika yeye [Yaani Kristo], mbele ya msingi wa ulimwengu” (Waef 1:4). Katika kipindi cha historia ya ulimwengu, Mungu kwa ufanisi anawaita wateule wake wote kutoka giza la dhambi na laana ndani ya “mwili mmoja” wa Yesu Kristo. Hivyo, watu wote waliochaguliwa na Mungu wanabatizwa kirohokwa “ubatizo mmoja.” “Kwa maana kwa Roho mmoja sisi sote tulibatizwa katika mwili mmoja” (1 Wakor. 12:13).

Roho Mtakatifu hukaa ndani ya Kristo, kichwa, na hivyo kwa waumini kama viungo vyake, kwa sababu “mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake” (Warum. 8:9). “Roho mmoja” katika waumini wote huthibitisha ukweli wa Neno la Mungu, na hivyo Wakristo wa kweli hupokea kila kitu kinachofunuliwa katika Maandiko Matakatifu (“imani moja”). Vile vile, watu wa Mungu wanashiriki “tumaini moja,” na hivyo, kwa “Roho mmoja,” tunatazama na kuomba na kutamani “kufunuliwa kwa utukufu wa Mungu mkuu naMwokozi wetu Yesu Kristo” (Tito 2:13).

Yesu Kristo ni “Bwana mmoja” wa kanisa ambaye anammiliki na ana mamlaka kamili juu yake, kwa kanisa si lake mwenyewe lakini ni mali ya Mwokozi wake mwaminifu ambaye alimnunulia kwa damu yake mwenyewe ya thamani. Kristo, aliye Bwana pekee wa kanisa, aliyewakomboa, anamwita, anamfanya kuwa “mwili mmoja,” anamfanya kuwa hai kwa “Roho Wake mmoja,” na kumpa “imani moja,” “tumaini moja” na “ubatizo mmoja.”

Muungano wa Kanisa ni hili, na hili peke yake. Umoja wa Kanisa hautapatikana katika makanisa ambayo kwa kweli hayakubali uongozi wa Kristo katika mambo yote lakini yanageuka kando na “imani moja” na “tumaini moja” la Maandiko kwa njia ya mapatano na dhambi na ulimwengu na Makanisa ya uongo. Wala umoja wa kanisa hautegemei maoni ya pamoja ya kisiasa au cheo cha kawaida katika jamii. Umoja wa Kanisa la Kristo umevuka mipaka na kushinda tofauti zote za dunia: tabaka, rangi, jinsia, umri, na kadhalika, kwa sababu “Hakuna Mgiriki wala Myahudi, tohara wala kutokutahiriwa, Kibabaria, Msikithe, kifungo wala huru; bali Kristo ni yote, na katika yote” (Wakol 3:11).

Umoja huu wa kanisa ni ukweli. Hivyo Roho anatangaza, “Kuna mwili mmoja;” si, “Utaumba mwili mmoja.” Umoja wa Kanisa si kwa kuumbwa na sisi, maana ni zawadi ya neema tukufu ya Mungu. Badala yake, kanisa limeitwa “kutunza” na “umoja wa Roho katika kifungo cha amani” (Waef 4:3). Hii inafanywa na waaminio, wakikiri na kushikamana na “imani moja” na “tumaini moja” la “Bwana mmoja” kwa “Roho mmoja;” na kwa waumini kwa moyo mmoja na kwa furaha wakitumia vipawa vyao kwa faida na wokovu wa viungo vingine vya “mwili mmoja” katika “unyenyekevu,” “upole” na “upendo” (Waef 4:2).

Show Buttons
Hide Buttons